Basata yataja mambo matano ya kuzingatiwa Swahili Fashion

Muktasari:

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limetoa maelekezo ya mambo matano ya kuzingatiwa katika onyesho la mavazi la Swahili Fashion ikiwemo kutodhalilisha utu wa watakaovaa  mavazi ya kupitia nayo jukwaani.

Dar es Salaam.Baraza la Sanaa la Taifa(Basata), limetoa maelekezo ya mambo matano ya kuzingatiwa katika onyesho la mavazi la swahili fashion linalotarajiwa kuanza Novemba 30  hadi Desemba 2 mwaka huu.
Akizungumza leo Novemba 2, katika mkutano na waandishi wa Habari kuhusu onyesho hilo litakalofanyika Makusho ya Taiga jijini humo,Mkurugenzi wa Promosheni ya Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua, ameyataja masharti hayo kuwa ni pamoja na kuangalia Tamaduni zetu za kiswahili.
"Hapa nieleweke sisemi kwamba msiige kutoka tamaduni nyingine kwani ni vizuri kuchanganya mitindo lakini tuhakikishe katika  kuiga huko hatupotezi utamaduni wetu.
Pia jingine ni kuhakikisha kila tunachokifanya katika onyesho hilo linaakisi uswahili wetu, kwani itasadia kukuza hata lugha yetu.
Vilevile baraza hilo limewataka wabunifu katika onyesho hilo kutumia  vitambaa vinavyotengenezwa hapa nchini  ikiwemo kanga zenye maneno mbalimbali ya kiswahili ambayo mtu atapenda kujua maana yake na pia kutangaza bidhaa za hapa nyumbani .
Kuhakikisha wabunifu wanaoshiriki Swahili fasheni wote wanakuwa wamejisajili na baraza hilo bapo hii itasaidia   kuondoa lawama kuwa Mustafa amekuwa akipendelea baadhi ya watu kushiriki onyesho hilo kila mwaka.
Kwa upande wake muasisi wa onyesho hilo, Mustafa Hassanali, amesema shindano hilo linaingia mwaka wa 11 sasa tangu kianza kwake na mwaka huu jumla ya wabunifu 50 wataonyesha mAvazi yao, 20 wakiwa  kutoka nchi za nje.

Hasannal amesema kwao huchukulia kama Sanaa ni biashara na sio burudani, hivyo anaamini kupitia jukwaa hilo wabunifu wanaweza kujitangaza na hatimaye kufanya biashara.