Barcelona yaibuka na mpya dili la Neymar

Tuesday August 13 2019

 

Madrid, Hispania . TAARIFA ni kwamba Barcelona imeamua kujikita vilivyo katika mbio za usajili wa Neymar na safari hii wametoa ofa ya kumtoa Philippe Coutinho pamoja na Pauni 55 milioni kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo.
 Neymar ameshaweka wazi kwamba ‘lazima’ aondoke kambi  Parc des Princes na yupo katika vita kubwa na viongozi wake baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu wakati wa mapumziko ya ligi.
 Imefahamika kuwa Barcelona hawapo tayari kutoa kiasi cha Pauni 200 milioni ambazo PSG wanazihitaji kwa kuwa katika siku za karibuni wamelipa kiasi cha Pauni 108 na kumnasa Antoine Griezmann  lakini wapo tayari kuongeza mchezaji kutoka katika dili hilo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa mpango wa kulipa Pauni 55 milioni na mchezaji mmoja huenda usifanikiwe na kwamba kama wakiongeza mpaka Pauni 74 mioni pamoja na   Coutinho wanaweza kusikilizwa.

Advertisement