Barcelona sasa yahamia kwa Lindelof

Muktasari:

Wababe hao wa Catalunya wamechemsha katika mbio za kumnasa De Ligt ambaye awali walikuwa na na matarajio makubwa ya kumnasa beki huyo aliyefanya vizuri akiwa na klabu yake ya Ajax.

BARCELONA imeelekeza nguvu zake kwa beki wa kati wa Manchester United, Victor Lindelof baada ya kushindwa kumnasa beki wa Ajax na Timu ya Taifa ya Uholanzi, Matthijs de Ligt ambaye alikuwa chaguo lake la kwanza.

Baada ya kuanza kusuasua Old Trafford, Lindelof ambaye alinunuliwa kutoka Benfica mwaka 2017 kwa dau la Pauni 31 milioni alikuwa chaguo la kwanza Manchester United msimu uliopita na Barcelona imevutika na kiwango chake.

Wababe hao wa Catalunya wamechemsha katika mbio za kumnasa De Ligt ambaye awali walikuwa na na matarajio makubwa ya kumnasa beki huyo aliyefanya vizuri akiwa na klabu yake ya Ajax.

Inadaiwa dau la Matthij de Ligt na mshahara wake limekuwa kubwa na sasa staa huyo anakaribia kutua Juventus baada ya kukubaliana nayo maslahi binafsi. Supastaa Cristiano Ronaldo aliwahi kumshawishi beki huyo kutua Juve.