Barcelona na PSG zapigana vikumbo kwa Antonio Rudiger

 PARIS Saint-Germain, West Ham na Barcelona zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya beki wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger katika dirisha hili.

PSG ndio inaonekana kuwa kwenye nafasi kubwa ya kuipata saini yake kwa kuwa ni ngumu Chelsea kuiuzia mchezaji West Ham kutokana na ushindani wa muda mrefu uliopo baina yao.

Katika kufanikisha hilo PSG imeripotiwa kutaka kumchukua mwamba huyo kwa mkataba wa mkopo ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja ikiwa ataonesha kiwango kikubwa.

Mchezaji huyo ambaye pia anawindwa na Barcelona hayupo kwenye mipango ya Frank Lampard kwa msimu huu. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2022 thamani yake katika soko la usajili ni Euro 40 milioni. Kukosa kwake namba kunamfanya ajiweke tayari kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine.