Barcelona kumpeleka Dembele Man United ili kumpata Pogba

BARCELONA inaweza kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi katika kuboresha safu yao ya kiungo ambayo inaonesha kupwaya katika misimu kadhaa.

Usajili huo wa Pogba unaweza kukamilika kwa Ousmane Dembele kutua Man United ikiwa sehemu ya mabadilishano ya wachezaji kama ilivyoripotiwa.

Barca kwa sasa imeyumba kiuchumi hali inayosababisha ishindwe kufanya usajili kwa kutumia pesa hivyo ili kuhakikisha inaipata saini ya Pogba italazimika kumuachia Dembele ambaye Man United inaitamani saini yake kwa muda mrefu na dirisha lililopita ilifeli katika dakika za mwisho.

Mkataba wa Pogba unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 thamani yake katika soko la usajili ni Euro 80 milioni, mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango cha kupanda na kushuka kwa muda mrefu.