Bao la Shija mkina laleta kizaazaa Nyamagana

Saturday November 9 2019

By James Mlaga, Mwanza

BAADA ya mshambuliaji wa Pamba, FC Shija Mkina kufunga bao dakika ya 26 kwenye mchezo wa Ligi Daraja la kwanza Kundi B dhidi ya Green Warriors katika dimba la Nyamagana Jijini hapa, mambo ghafla yakabadilika kwani mchezo ukalazika kusimama  kwa dakika 10.

Mambo yalikuwa hivi, Mkina aliipokea krosi kutoka kwa Siprian Mtesigwa ambayo ilimkuta akiwa ndani ya Sita katika eneo la hatari la Green Warriors, baada ya hapo Mabeki wote walimuacha, akautuliza mpira baadae akaukwamisha wavuni.

Baada ya bao hilo, Wachezaji wote wa Green Warriors pamoja na Viongozi wao na baadhi ya Mashabiki ambao wanaiunga mkono timu hiyo, walianza kutupa maneno kwa Waamuzi kwamba bao sio halali kwani Nyota huyo alikuwa ameotea.

Licha ya Waamuzi kukomalia maamuzi yao ya kuweka mpira kati, Wachezaji waliendelea kugomea jambo hilo, jambo ambalo lilipelekea mchezo kusimama kwa takribani dakika 10.

Baada ya dakika hizo kuisha mambo yakatulia na timu zote zikakubaliana kuwa mpira uwekwe kati jambo ambalo limepelekea Pamba kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0 .

Advertisement