Bandari FC yapania kuvuna alama tatu kwa AFC Leopards

Muktasari:

  • Bandari FC itahitaji kuhakikisha inapata pointi zote tatu itakapokutana na AFC Leopards katika pambano litakalofanyika Jumapili wikiendi hii.

BANDARI FC baada ya kuilaza kwa bao 1-0 na Gor Mahia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya SportPesa iliyofanyika Uwanja wa Moi mjini Kisumu, sasa itahitaji kuhakikisha inapata pointi zote tatu itakapokutana na AFC Leopards katika pambano litakalofanyika Jumapili wikiendi hii.

Naibu Kocha wa Bandari FC, Nassor Mwakoba aliliambia Mwanaspoti kuwa baada ya kumalizika kwa mechi yao na Gor kuwa mchezo huo walipoteza kwenye dakika ya majeruhi kutokana na wapinzani wao hao kutumia nafasi yao nzuri ya kufunga.

“Kwa uhakika mchezo wenyewe ulikuwa 50-50 kwani timu zetu mbili ziliweza kukabiliana vilivyo. Gor ilifanikiwa kutumia nafasi yao nzuri waliyopata na kuweza kuondoka kiwanjani wakiwa washindi,” akasema Mwakoba.

Mkufunzi huyo alisema kutokana na kushindwa huko, watajitahidi kuhakikisha wanapata ushindi watakapokutana na Leopards hapo Jumapili kwenye uwanja ambao ulikuwa haujafahamika. “Tunasubiri tuambiwe ni kiwanja gani tutakachochezea,” akasema.

Mwakoba alisema timu yake iko imara na itapambana na Leopards ikiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi. Kwa siku zilizobaki, tutafanya kazi ya kurekebisha makosa madogo yaliyofanyika dhidi ya Gor ili tupate kurudi nyumbani na pointi tatu,” akasema.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Admiral Youth FC, Aref Baghazally alisema ratiba ya mechi za Ligi Kuu ya SportPesa na SportPesa Shield zinaumiza wachezaji kwa sababu ya kucheza mechi nyingi kwa kipindi kifupi.

Baghazally aliomba Kenya Premier league (KPL) na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) zifanye kuandaa mechi za ligi mapema na kutoa nafasi nzuri kwa wachezaji kucheza mechi zao huku wakipata fursa ya mapumziko.

“Kucheza mechi mfululizo kunaumiza wachezaji na hata kunaweza kuwafanya wanasoka kuumia vibaya. Timu yetu ya Bandari imeumia sana kwa safari nyingi  na kucheza mechi mfululizo,” akasema Baghazally.