Bajaj SportPesa sasa yatua Kigoma

Muktasari:

Baba mzazi wa mshindi huyo, Joseph Mussa Fundi alisema ameupokea ushindi wa mwanae kwa furaha na kuamini kuwa taa ya ushindi imeweka katika familia yake.

PROMOSHENI ya Shinda Zaidi na SportPesa imeendelea kuchjanja mbuga baada ya wikiendi iliyopita, Amir Nicholas Junya, mkazi wa Kigoma Mwanga Majengo kukabidhiwa bajaji kufuatia kushinda droo ya 28 ya promosheni hiyo.

Junya alikabidhiwa bajaj yake hiyo na mwakilishi wa SportPesa mbele ya wazazi wake na majirani zake, huku akikiri kwamba ni mara yake ya kwanza kushinda bahati nasibu na kushukuru kunyakua zawadi hiyo.

“Kupitia bajaj hii, kwanza kabisa nina uhakika ndani ya mwaka mmoja kununua kiwanja ili kujenga nyumba yangu, kwani kwa sasa naishi nyumbani kwa wazazi,

pia nataka kuanza biashara ya kuuza dagaa,” alisema mshindi huyo.

Baba mzazi wa mshindi huyo, Joseph Mussa Fundi alisema ameupokea ushindi wa mwanae kwa furaha na kuamini kuwa taa ya ushindi imeweka katika familia yake.

“Mwanangu aliniambia bajaj iko njiani na sikuamini, ila leo nimeamini na hata wadogo zake wakija kuniomba pesa ya kucheza ntawapa ili wavune ushindi tena, si unaona umri wangu unaenda, najua mwanangu atanitunza vyema kutokana na kipato atakachopata kutoka kwa bajaji tunashukuru sana SportPesa “ alisema.

Promosheni hiyo inamwezesha mteja kushinda kama tu atajisajili kupitia simu yako ya mkononi kwa kupiga *150*87# na kuweka pesa kwa kubonyeza namba 7 na kuanza kucheza. SportsPesa ilitenga bajaj 100 kwa promosheni hiyo ya kijanja.