Bafana Bafana yajificha kwao

Muktasari:

  • Hilo limebainika wakati Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stuart Baxter alipotangaza kikosi cha wachezaji 30 ambao wataingia kambini jijini Johannesburg kuanzia Juni 2 hadi 12 watakaposafiri kwenda Misri.

TIMU ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ haitoweka nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na Fainali za AFCON) mwaka huu.

Nchi mbalimbali ambazo zitashiriki fainali hizo zimepanga kuweka kambi zao za maandalizi nje ya nchi hasa barani Ulaya na Mashariki ya Kati lakini Afrika Kusini wenyewe wameamua kubaki nyumbani kujiandaa na fainali hizo.

Hilo limebainika wakati Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stuart Baxter alipotangaza kikosi cha wachezaji 30 ambao wataingia kambini jijini Johannesburg kuanzia Juni 2 hadi 12 watakaposafiri kwenda Misri.

Makipa walioitwa ni Darren Keet (Bidvest Wits), Ronwen Williams (Supersport United) na Bruce Bvuma (Kaizer Chiefs) wakati mabeki ni Daniel Cardoso (Kaizer Chiefs), Rivaldo Coetzee (Mamelodi Sundowns), Ramahlwe Mphahlele (Kaizer Chiefs), Thulani Hlatshwayo (Bidvest Wits), Innocent Maela (Orlando Pirates), S’Fiso Hlanti (Bidvest Wits), Buhle Mkhawanazi (Bidvest Wits) na Thamsanqa Mkhize (Cape Town City).

Viungo yupo Daniel Cardoso (Kaizer Chiefs), Rivaldo Coetzee (Mamelodi Sundowns), Ramahlwe Mphahlele (Kaizer Chiefs), Thulani Hlatshwayo (Bidvest Wits), Innocent Maela (Orlando Pirates), S’Fiso Hlanti (Bidvest Wits), Buhle Mkhawanazi (Bidvest Wits) pamoja na Thamsanqa Mkhize (Cape Town City)

Washambuliaji kuna Lebo Mothiba (Strasbourg), Percy Tau (Royal St. Union), Lars Veldwijk (Sparta Rotterdam), Lebogang Maboe (Mamelodi Sundowns), Sibusiso Vilakazi (Mamelodi Sundowns) na Kermit Erasmus (Cape Town City).