BDF ya Mandawa kujipanga upya

Monday January 7 2019

 

BAADA ya BDF XI kuumaliza vibaya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Botswana, mshambuliaji wa Kitanzania, Rashid Mandawa amesema wanatakiwa kufanya kazi ya ziada katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
BDF XI imeamliza vibaya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Gaborone United.
“Mzunguko wa pili siku zote ndio unaoamua nani anaweza kuwa bingwa, utofauti wetu wa pointi na timu inayoongoza kwenye ligi ni mdogo kwa hiyo inatakiwa tukaze,” alisema Mandawa.
Katika mzunguko wa kwanza, BDF XI, imepoteza michezo mitatu, ukiwemo iliochapwa na Gaborone United, imeshinda saba na kwenda sare kwenye michezo mitano.
Timu hiyo ya Mandawa imejikusanyia pointi 26 kwenye michezo 15 ya mzunguko wa kwanza, ipo nyuma kwa alama 10 ambazo imeachwa na vinara wa ligi hiyo, Township Rollers.

Advertisement