Azam yazidi kuziburuza Simba, Yanga, Mtibwa

Muktasari:

 Mpaka sasa wakati ligi ikiingia raundi ya 14,Azam ndio timu pekee iliyoruhusu mabao machache ikiwa imefungwa mabao mawili tu ikifutiwa na JKT Tanzania iliyoruhusu mabao matatu wakati Yanga na Simba zimeruhusu mabao manne kila mmoja.

Azam Fc imeonekana haitaki mchezo msmu huu baada ya kuzidi kuwaburuza watani wa jadi Simba na Yanga kwenye msimamo wa ligi ambazo zinakimbizana nafasi ya pili tatu zikiwa na alama 26 kila moja.
Licha ya kuwa Yanga na Azam ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo lakini wanalamba lamba hao wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa wiki ya sita sasa huku wakiwa hawana dalili ya kushuka.
Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza michezo 12,imeshinda 9,imetoa sare michezo mitatu na haijapoteza mchezo.
Pia Safu ya ulinzi ya timu hiyo inayoongozwa na kipa Razack Abalora imeonekana kuwa na ukuta wa chuma na haupitiki kirahisi kwani imeruhusu mabao machache.