Azam waifuatisha Yanga mechi ya Simba

Muktasari:

Kitendo cha Azam FC kutumia mlango huo kimeibua mjadala mkali kwa mashabiki kwamba endapo kama timu hiyo itaiga mambo ya Simba na Yanga itapotea.

 AZAM FC wamefanya kama Yanga kuingilia geti la kupitia magari ya dharula wakati wanaenda kupasha misuri tayari kwa mechi yao na Simba. Yanga wakati wanacheza na Simba waliingilia mlango huo walioutumia leo Azam FC na kujikuta wakizomewa na mashabiki wa Simba.

Kitendo cha Azam FC kutumia mlango huo kimeibua mjadala mkali kwa mashabiki kwamba endapo kama timu hiyo itaiga mambo ya Simba na Yanga itapotea.

Mwanaspoti liliwasikia wakisema "Azam haitakiwi kuiga mambo ya ovyo ya Simba na Yanga huo mlango ndio walioingilia Yanga wakati wanacheza na Simba na wakapigwa vile vile. "Hii inamanisha tayari wamejitoa mchezoni lakini pia wana kila kitu wanapaswa kuonyesha soka safi ila wakianza hivi watapotea Tanzania tutaendelea kufanya ovyo kwenye mpira wa miguu"walisikika wakijibizana.

Kocha Hans Pluijm ndiye akikuwa wa mwisho kuingia uwanjani hakuonekana kusumbuka sana na zomea za ya mashabiki wa Simba. Lakini pia straika wa timu hiyo Obrey Chirwa ndiye alikuwa wa kwanza kuingia uwanjani wakati kwa upande wa Simba alikuwa ni Aishi Manula aliyepitia pembeni ya kibendera.

Mashabiki wanaendelea kumiminika uwanjani ingawa msisimko wake sio mkubwa kama ilivyokuwa mechi yaYanga na Simba.