Azam kutetea taji Kigali

Muktasari:

  • Marais wa mashirikisho yaliyo chini ya CECAFA, walikutana mjini Adis Ababa, Ethiopia Jumatatu wiki hii na kuafikiana kufanikisha kalenda hii mpya.

NAIROBI.WATETEZI wa Kombe la Kagame kwa misimu miwili mfululizo, Azam watakuwa na kazi ya kutetea taji hilo kwa mara ya tatu mjini Kigali, Rwanda baada ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kutangaza ratiba yao ya mwaka.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye alisema michuano yote itachezwa kuanzia Juni hadi Desemba katika nchi za Rwanda, Tanzania, Kenya, Eritrea na Uganda.

Marais wa mashirikisho yaliyo chini ya CECAFA, walikutana mjini Adis Ababa, Ethiopia Jumatatu wiki hii na kuafikiana kufanikisha kalenda hii mpya.

Viongozi hao walikuwa katika shughuli za kufungua ofisi ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ya kanda hii.

“Eritrea itaandaa CECAFA U17 huku Kenya ikiwa mwenyeji wa U17 ya kina dada kisha Chalenji ya Wanawake itafanyika nchini Tanzania nayo U-20 ya kina dada nchini Uganda,” alisema Musonye.

“Michuano ya Kombe la Kagame inayofadhiliwa na Azam TV na rais wa Rwanda Paul Kagame itapigwa kule Kigali kisha Chalenji ya wanaume nchini Uganda mwezi Desemba,” aliongeza Tanzania wamethibitisha kuandaa U-17.