Azam akili yote ipo CAF

Muktasari:

  • Azam na Lipuli zitavaana Juni Mosi kuwania tiketi ya CAF ya kuiwakilisha nchi katikati ya mwaka huu.

NAHODHA Azam FC, Aggrey Morris amesema akili yao yote wameielekeza katika mechi ya Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Lipuli wakiwa na kiu ya kutaka kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Morris alisema mechi hiyo, kwao ndio muhimu kuliko hata mechi mbili za kukamilishia ratiba ya Ligi Kuu Bara kwani, tayari bingwa na hata mshindi wa pili ameshapatikana.

Azam na Lipuli zitavaana Juni Mosi kuwania tiketi ya CAF ya kuiwakilisha nchi katikati ya mwaka huu.

“Lipuli ni wazuri na ndio maana wameweza kuingia hatua hiyo siwezi kumhofia mchezaji mmoja katikati ya kikosi cha nyota 11 nawaheshimu nyota wote na naamini ni bora lakini hawawezi wakawa bora zaidi yetu, kikubwa naweza kusema dakika 90 zitaamua nani ni bora zaidi ya mwingine, kwani tunitaka tiketi ya CAF,” alisema.

Kuhusu Ligi Kuu alisema wana mechi mbili za kukamilishia ratiba na wanataka kumaliza kwa heshima kwa kupata matokeo mazuri katika michezo yote watakayocheza nyumbani, lakini kubwa kwao ni fainali ya FA.