Azam FC wasapoti mechi ya waandishi

Muktasari:

Mechi ya waandishi wa habari za michezo wale walio kwenye ndoa na wale wasio kwenye ndoa, itachezwa Jumapili, Juni 31 katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo Mawasiliano jijini kuanzia saa 4.00 asubuhi.

Uongozi wa Azam FC, umetoa katoni za maji kwa waandishi wa habari za michezo nchini kwa ajili ya kusapoti mechi baina yao itakayochezwa Jumapili saa 4.00 asubuhi katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini.   

Mechi hiyo itakuwa ni baina ya waandishi wa habari za michezo walio kwenye ndoa na wale ambao hawapo kwenye ndoa.

Meneja Utawala wa Azam FC, Hamis Jecha alisema wamefanya hivyo ili kuonesha usirikiano wao na Waandishi wa habari za michezo.

"Unajua hili jambo ni letu kwani hawa waandishi huwa tunashirikiana nao kila siku katika majukumu ya kuwapa habari za Azam FC wapenzi wetu," anasema.

"Kwa maana hiyo hiki ambacho tumejaliwa katika mechi hii ndio tumekifanikisha kukitoa hapa  na tunaimani wakati mwingine watakuja kucheza waliooa zamani na waliooa wakati wa sasa," alisema Jecha.