Azam, KMC yashuhudiwa na mashabiki kiduchu

Muktasari:


Mechi hizo zote zimeanza saa10:00 jioni Azam FC na KMC zikiwa zinacheza Uwanja wa Taifa, ambako mashabiki walikuwa wa kuhesabu.

MECHI ya Azam FC na KMC imeshuhudiwa na mashabiki kiduchu, huku upande wa pili Uwanja wa Uhuru, ambapo inachezwa mechi baina ya Yanga na Ruvu ikiwa imezaja nyomi ya watu.

Mechi hizo zote zimeanza saa10:00 jioni Azam FC na KMC zikiwa zinacheza Uwanja wa Taifa, ambako mashabiki walikuwa wa kuhesabu.

Licha ya mashabiki kuwa wa kuhesabu wapo wale ambao wameonekana kuvalia jezi ya timu ya Yanga ambao ndio walikuwa wengi kidogo, waliobakia walivaa jezi za  Azam FC na KMC.

Imeonekana changamoto kucheza mechi muda mmoja na viwanja vipo karibu ambapo Yanga na Ruvu ndio inaonekana kuwa na amsha amsha ya mashabiki.

Kuna mashabiki kindaki ndaki wa Azam FC na KMC ambao walionekana kupiga ngoma huku wakikosa watu wa kucheza na kuimba kama ilivyo kawaida yao.

Azam FC ilikwenda mapumziko kwa ushindi wa mabao 3-0, mawili yakifungwa na Obrey Chirwa na Djodji Richard ambaye alitoa pasi ya bao la pili.