Aussems: Yanga, Azam FC ilikuwa wiki ya ngumu

Muktasari:

Amesema, baada ya michezo hiyo imeshapita, wanarudi barabarani kama kawaida kufanya maandalizi ya mchezo ujao.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amesema, wamepita kwenye wiki ngumu lakini yenye furaha kwao.

 Aussems amesema, walicheza mechi ngumu ya Yanga na hii ya Azam FC lakini anashukuru wameshinda.

Kocha huyo maarufu kwa jina la Uchebe kutokana na staili yake ya kufuga ndevu ndefu kidevuni mwake.

Amesema, baada ya michezo hiyo imeshapita, wanarudi kama kawaida kufanya maandalizi ya mchezo ujao.

 "Muhimu na malengo ni pointi tatu, tunashukuru tumeshinda mchezo wetu na Azam tunasonga mbele, " alisema Aussems. Simba watakuwa ugenini kucheza na Lipuli FC wiki ijayo Uwanja wa Samola Iringa.