Aubameyang, Ozil waonywa

Muktasari:

Aubameyang na Mesut Ozil. Wachezaji hao wametakiwa kusaini mkataba mpya au kuondoka mapema kwa kuwa wamebakisha miaka miwili katika mikataba yao.

LONDON,England.Raul Sanllehi wameweka wazi wanataka kufanya mambo makubwa katika dirisha la usajili linalokuja ili kuleta mapinduzi katika klabu yao. Wamesema licha ya kwamba watakuwa na kiasi kidogo cha pesa za usajili watajitahidi kuwa makini katika kuuza wachezaji na kutumia pesa vizuri.

Wamesema kinachowafanya kuwa makini zaidi ni ukweli hawataki kurudia hasara ambayo walipata kwa nyota wawili Alexis Sanchez na Aaron Ramsey. Wachezaji hao walikuwa wakisuasua katika kuongeza mkataba na matokeo yake wakaondoka wakiwa huru jambo ambalo liliwapa hasara kubwa.

Huku Kocha Unai Emery akiwa katika harakati za kutafuta nyota wa kuifanya timu itambe, onyo limetolewa kwa wachezaji wawili

Pierre-Emerick

Aubameyang na Mesut Ozil. Wachezaji hao wametakiwa kusaini mkataba mpya au kuondoka mapema kwa kuwa wamebakisha miaka miwili katika mikataba yao.

Sanllehi alisema “Tunatakiwa kuwa makini sana. Hatutaki mambo ya Sanchez na yajirudie. Wachezaji hao waliondoka katika klabu wakati mikataba yao imekwisha, hiyo ilitupa hasara, waliondoka wakiwa huru.

“Sasa Aubameyang na Mesut Ozil wamebakiza miaka miwili katika miakataba yao, wanatakiwa wafanye maamuzi ya haraka. Wanataka wauzwe ama wakubali kusaini mkataba mpya.”

“Na hili suala halitaishia kwa wachezaji hao tu, kila mara tutakapokuwa na hali kama hiyo, itabidi wachezaji wafanye maamuzi ya mapema.”