Arsenal wenyeji wa Napoli Uefa Europa League

Friday March 15 2019

 

By Nyon, Uswisi

Klabu ya Arsenal itacheza na Napoli mechi ya robo fainali ya Uefa Europa League mchezo ambao ni baada ya droo hiyo kufanyika leo Ijumaa.
Mbali na mchezo huo, Slavia Praha watakuwa wenyeji wa Chelsea,
Benfica itacheza na Eintracht wakati Villarreal watawakaribisha
Valencia.
Katika mechi hizo ambazo zinachezwa nyumbani na ugenini zitapigwa siku moja ya Aprili 11 katika viwanja vinne tofauti.
Katika fainali hizo bingwa mtetezi ni Atretico Madrid ambao waliyaaga mapema mashindano hayo.
Katika hatua nyingine droo ya robo fainali ya Klabu Bingwa Bara la Ulaya (UEFA Champion League) imefanyika leo Ijumaa Nyon, Uswisi ambapo mechi kali ikitajwa kuwa kati ya Barcelona na Manchester United.
Manguli hao wa soka barani Ulaya watacheza mchezo wa kwanza
katika Uwanja wa Old Trafford, England na Manchester United
atakuwa mwenyeji.
Mechi nyingine Liverpool atawakaribisha FC Porto kwenye Uwanja
wa Anfield, Ajax itakuwa nyumbani kukipiga na Juventus wakati
Tottenham Hotspour watakuwa wenyeji wa Manchester City na mechi hizo zitachezwa nyumbani na ugenini.
Katika michuano hiyo, Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi, waliyaaga mapema mashindano hayo.
Madrid chini ya Kocha Zinedine Zidane imechukua mara tatu
mfululizo na alipoondoka tu, ikaanza kutetereka kwa kupata
matokeo mabaya.
Siku tatu zilizopita, Real Madrid imemrudisha nyumbani Zinedine
kuendelea na majukumu yake.

Advertisement