Arsenal nao wamtaka Toby Alderweireld

Monday April 15 2019

 

ARSENAL inataka kufanya uhamisho wa kushtukiza kwa kumchukua beki wa wapinzani wao wa jadi, Tottenham Hotspurs, Toby Alderweireld ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Manchester United.

Staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anaruhusiwa kuondoka Tottenham kwa dau la Pauni 25 milioni tu kwa mujibu wa kipengele cha mkataba wake na Arsenal imeingia katika mkumbo wa kuliona dau hilo ni rahisi kuliko ilivyo kwa walinzi wengine walio sokoni.

Endapo Toby atakwenda Arsenal atakuwa amefuata nyayo za beki wa zamani wa Kimataifa wa England, Sol Campbell ambaye mwaka 2001 alitua Arsenal akitokea Tottenham katika uhamisho huru ambao ulimjengea chuki kutoka kwa mashabiki wa Spurs mpaka leo.

Safu ya ulinzi ya Arsenal bado haijakaa vizuri na kocha wa timu hiyo Unai Emery ameanza mikakati ya kukiweka sawa kikosi chake kwaajili ya msimu ujao.

Advertisement