Arsenal kupigwa mnada?

Wednesday August 8 2018

 

By Amani Njoka

Zinaweza kuwa ni habari zitakazowashtua mashabiki wa Arsenal au zisiwashtue kwa sababu pengine klabu haitabadilika kwa kiwango cha wagusa moja kwa moja mashabiki. Arsenal muda wowote kuanzia sasa inaweza kuwa mikononi mwa mtu mmoja kwa asilimia 100. Imefichuka kuwa kampuni Kroenke Sports&Entertainment chini ya bosi wake Stan Kroenke ipo tayari kuzinunua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na tajiri Alisher Usmanov.

Kampuni hiyo kutoka nchini Marekani ambao ndiyo wamiliki ndiyo wamiliki wakuu wa Arsenal wameshaweka tayari kitika cha dola za Kimarekani bilioni 1.8 kwa ajili ya kubeba asilimia 100 ya hisa zote za Arsenal.

Inasemekana kuwa Usmanov ndiye alikuwa wa kwanza kujaribu kununua hisa zote zote  kwa mahasimu wake sasa ataweka kibindoni kiasi cha Dola milioni 550 kama gawio lake. KSE na Delaware kwa pamoja ambayo inamilikiwa na Bw. Stanley Kroenke kwa sasa wanamiliki hisa zaidi ya 41,000 ambazo zinakadiriwa kuwa ni sawa na asilimia 67.09 ya hisa zote za Arsenal.

Inadaiwa kuwa Kroenke alipokea taarifa kutoka kwa bilionea huyo wa Kirusi mwenye asili ya Uzbekistan kuwa anataka kuuza asilimia 30 aliyokuwa anaimiliki katika klabu ya Arsenal. Taarifa kutoka KSE zinasema kwamba Kroenke aliazimia kwamba “ sisi kama KSE tunasonga mbele tukiitazama ofa hii ambayo itatufanya tumiliki asilimia 100 ya klabu.”

 

 “Tunatambua vyema mchango wa Bw. Usmanov kwa klabu ya Arsenal tangu alipoanza mpaka hapa alipofikia” aliongeza. Hata hivyo, licha ya kwamba Usmanov (pichani) alikuwa ni wa pili kwa umiliki wa hisa nyingi ndani ya klabu ya Arsenal, hakuwahi kupewa nafasi yoyote katika bodi ya klabu hiyo.

 

Kroenke atalazimika kulipa kiasi cha Dola 29,419.64 kwa kila hisa ya Arsenal ili kuichukua moja kwa moja chini ya kampuni yake, ambayo pia inamiliki timu ya Ragbi (NFL)  LA Rams, timu ya mpira wa kikapu (NBA) Denver Nuggets, timu ya mpira wa miguu ya ligi ya Marekani (MLS) Colorado Rapids pamoja na ile ya mpira wa magongo (NHL) Colorado Avalanche.

Hii haijawa mara ya kwanza kwa Kroenke na kampuni yake kuinunua klabu ya Arsenal kwani mwaka 2011 waliweka mezani kitita cha Dola milioni 528 ili wanunue hisa zaidi ya 18,000 ambazo zinamilikiwa na Usmanov lakini zilikataliwa.

Tangazo hili la hisa za Usmanov kuuzwa zilitangazwa rasmi asubuhi ya Jumanne ya leo na soko la hisa la mjini London, Uingereza. Kroenke Sports & Entertainment waliianza kuwekeza katika klabu ya Arsenal kwa kununua wachezaji, kuwalipa mishara wafanyakazi wote ambao ni pamoja na wachambuzi mbalimbali wa klabu ya Arsenal.

KSE wanasema kwamba wanataka kuiona timu katika kiwango cha ushindani kwa msimu ujao na hii ni pamoja na kubeba taji la ligi kuu pamoja na taji la ligio ya mabingwa barani Ulaya [amoja na mataji mengine. Waliongeza kuwa wanataka kuona timu zote za Arsenal zikifanikiwa, yaani timu ya mpira za mpira wa miguu wa vijana, wakubwa pamoja na wanawake.

Arsenal itaanza ligi wikiendi hii kwa kuwakaribisha Manchester City nyumbanbi kwao, Emirates. Ikumbukwe kuwa Arsena wameshindwa kuwafunga Manchester City katika michezo 5 ya hivi karibuni kwa kufungwa michezo 3 na kutoa sare 2. Kwa hiyo, Arsenal itakuwa na mlima mrefu wa kupanda ikiwa chini ya kocha wake mpya, Unai Emery.