Arsenal kumtoa Elneny na £40milioni kumpata Zaha

Friday July 12 2019

 

LONDON, ENGLAND.ARSENAL wametoa ofa ya Pauni 40 milioni pamoja na wachezaji watatu akiwamo kiungo wa Misri, Mohamed Elneny kwa klabu ya Crystal Palace ili kumpata Wilfried Zaha.
Ofay a awali wa The Gunners ya Pauni 40 milioni ilikataliwa na Palace, ambao wanataka Pauni 80 milioni kwa ajili ya nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ivory Coast.
Katika jaribio lao la kupunguza gharama ya pesa taslimu, kocha Unai Emery yuko tayari kumtoa Calum Chambers, Carl Jenkinson na Elneny ambao wanathaminishwa kama nusu ya bei ya Zaha.
Zaha aliongeza mkataba wake wa kubaki Selhurst Park kwa kusaini dili la miaka minne Juni mwaka jana.

Advertisement