Arsenal ikiihofia tu Man United imepigwa!

Wednesday December 5 2018

 

London, England. Kikosi cha Arsenal kinashuka ugenini leo kwenye Uwanja wa Old Trafford kuikabili Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo utapigwa leo Jumatano saa tano usiku mechi hiyo ikionekana kuziweka timu hizo katika vita ya kujiweka vema katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Man United ambayo inayonolewa na kocha Jose Mourinho itapewa sapoti zaidi na mashabiki wake kwenye dimba la Old Trafford.

Kwa mara ya mwisho Arsenal iliifunga Manchester United mchezo wa Ligi Kuu England Septemba mwaka 2006.

Arsenal inaingia kwenye mchezo huo ikijiamini kutokana na ujasiri iliopata baada ya kuifunga Tottenham katika mchezo wake uliopita.

Kocha Unai Emery atakuwa uwanjani akihitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kuwapo nne bora ambapo zinafukuzana Man City, Liverpool, Chelsea huku Tottenham ikiwa nafasi ya tano na alama 30 sawa na Arsenal.

Advertisement