Arsenal, Wolves wafanya kweli Ulaya

Muktasari:

Katika mechi ya Arsenal bao pekee la mchezo huo wa ugenini liliwekwa kimiani na Alexandre Lacazette dakima ya 81.

LONDON, England . KLABU za Wolves na Arsenal za England zimefanya kweli kwenye michuano ya Ligi ya Ulaya (UEFA Europe League) kwa kupata ushindi kwenye mechi zao zilizopigwa usiku wa kuamkia leo.
Arsenal wakiwa ugenini nchini Ugiriki, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Olympiacos Piraeus katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Georgios Karaiskakis, huku mjini Wolverhampton, Wolves iliwanyoa wageni wao, Espanyol ya Hispania kwa mabao 4-0.
Mabao ya Wolves yaliwekwa kimiani na Diogo Jota aliepiga hat trick kwa mabao ya dakika ya 15, 67 na 81, huku jingine likiwekwa kimiani na Ruben Neves katika dakika ya 52.
Katika mechi ya Arsenal bao pekee la mchezo huo wa ugenini liliwekwa kimiani na Alexandre Lacazette dakima ya 81.
Ushindi wa timu hizo ni kama umepoza machungu ya timu za England kwenye michuano ya Ulaya baada ya katikati ya wiki hii, Liverpool na Spurs kupasuka kwenye Ligib ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid na RB Leipzig, kila mmoja akifungwa bao 1-0, Liver wakipigwa ugenini nchini Hispania na Coyz wakifa nyumbani mbele ya Wajerumani hao.
Katika mechi nyingine za Ligi ya Ulaya, Inter Milan ilipata ushindi ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Ludogorets, huku AS Roma ikishinda nyumbani 1-0 dhidi ya Gent na Mashetani Wekundu, Manchester Uniter ikiwa ugenini nchini Ubelgiji ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Club Brugge.
Anthony Martial nmdiye aliyeifungia Man bao la kuswazisha dakika tisa kabla ya mapumziko, baada ya wenyeji kutambulia kufunga mapema kwenye dakika ya 15 kupitia Emmanuel Dennis.
Matokeo mengine ya mechi hizo ni kama ifuatavyo; APOEL 0-3 Basel, AZ Alkmaar 1-1 LASK, Bayer Leverkusen 2-1 FC Porto, Rangers 3-2 Braga, Wolfsburg 2-1 Malmo FF, CFR Cluj 1-1 Sevilla, Eintracht Frankfurt 4-1 Salzburg, FC Copenhagen 1-1 Celtic, Getafe 2-0 Ajax, Shakhtar Donetsk 2-1 Benfica,
Sporting 3-1 Basaksehir.