Arachuga mzuka wa Yanga na Simba umekolea

Muktasari:

Bendera alisema kama waliwakosa Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Septemba 30, mwaka jana, basi safari hii Jangwani wasitarajie mteremko kutoka kwao.

NANI alikwambia homa ya pambano la watani lipo jijini Dar tu, huku mikoani nako mzuka umepanda ile kinoma na unaambiwa hata wale waliokuwa wameuchuna kwa muda mrefu ameamua kuvunja ukimya na kulizungumzia pambano hilo la 102 kwa watani hao tangu 1965.

Kocha wa zamani wa Simba, Madaraka Bendera ameipa ushindi timu yake akidai hakuna cha kuizuia kuifumua Yanga nyingi leo kwenye Uwanja wa Taifa.

Bendera alisema kama waliwakosa Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Septemba 30, mwaka jana, basi safari hii Jangwani wasitarajie mteremko kutoka kwao.

“Awali kipa wao, Beno Kakolanya aliokoa mashuti yote ya mashambulizi yaliyoelekezwa langoni mwao, lakini Simba ya awali si hii wanayodhania, hivyo hata sheria ingeruhusu wakaweka makipa wawili lazima kipigo wakipate tu,” alisema Bendera.