Andaa mkwanja mrefu kumuona Rick Ross

Thursday March 29 2018

 

UNATAKA kumuona Rick Ross jijini Nairobi? Basi wewe anandaa Sh3,000 za Kenya tu kumshuhudia rapa huyo mkali kutoka Marekani.

Taarifa zilizonaswa na Mwanaspoti zinasema, Rick Ross hivi karibuni amezima tetesi kuhusiana na ujio wake kupiga shoo nchini hapa.

Kwa mashabiki waliokuwa wakishuku taarifa hizo, The Big Boss sasa amethibitishia atatua nchini mwishoni mwa mwezi ujao ili kuwafurahisha mashabiki wake kwa kupiga shoo ya nguvu.

 Kupitia video fupi iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Ross amewatoa hofu mashabiki wake wanaomsubiria.

 “Vipi Nairobi kwa mara ya kwanza The Big Boss, Rick Ross natua mjini Aprili 28, nitawacheki nawahakikishieni itakuwa pati kubwa ya mabosi, itakuwa ni tamasha isiyo ya mfano itakuwa ni sherehe ya kipekee,” amekata kauli ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini ambapo ameahidi kupiga bonge la shoo litakalosalia kuwa kumbukumbu. Hata hivyo, kwa shabiki yeyote mwenye mipango ya kumcheki mkali huyo akifanya vitu vyake laivu katika Uwanja wa Carnivore Grounds Aprili 28, basi lazima awe tayari kulipia tiketi za gharama kubwa. 

Kwa wale watakaonunua tiketi za VIP kila mmoja atalipia Ksh9,0000  huku tiketi za kawaida zikiuzwa kwa Ksh3,000. Pia, kuna tiketi za kundi la watu wanne itakayouzwa kwa  Sh10,000.