Anasepa, atakapoenda Ozil Januari au Juni

LONDON, ENGLAND. NAFASI ya kiungo Mjerumani, Mesut Ozil katika klabu ya Arsenal imekuwa hafifu baada ya kocha Mikel Arteta kuonesha hayupo kwenye mipango ya kumtumia kwa msimu huu.

Arteta anaamini mchezaji huyo haendani na mifumo yake hali inayosababisha asimpe nafasi ya kucheza ikiwa msimu uliopita amecheza mechi 23 tu katika michuano yote.

Mbali na kuonekana hana nafasi ndani ya Arsenal, klabu nyingine zimeonesha nia ya kutaka kumsajili zikiamimi anaweza kuzisaidia zikafanya vizuri.

Mwanaspoti inakuelete orodha ya timu tano ambazo kiungo huyu anaweza kujiunga nazo katika dirisha lijalo la majira ya baridi au kiangazi.

DC United

Mwishoni mwa mwaka uliopita miamba hii ya Marekani ilionesha nia ya kutaka kumsajili lakini Arsenal haikuwa tayari kumuuza.

Kwa wakati huu inaweza ikawa klabu shindani kwenye kinyang’anyiro hichi kutokana na mshahara ambao wanaweza kuuweka kwenye ofa ya kuinasa saini yake.

Lakini jambo linalozidisha tetesi zaidi ni kitendo cha Arsenal kuwa kwenye mpango wa kutaka kuvunja mkataba wake jambo ambalo litakuwa ni furaha kwa DC United ambayo mara ya kwanza ilishindwa kutokana na bei iliyowekwa.

Saud

Arabia

Harakati za klabu kutoka nchini humu hazikuishia kwa Juan Mata tu, pia kuna ofa zilizowasilishwa kwenye meza ya Arsenal ikiwa ile ya Pauni 5 milioni kutoka Al-Nassr ambayo ilikataliwa.

Hapa ni sehemu nyingine ambapo mchezaji huyu anaweza kutua katika dirisha lijalo la majira ya baridi au kiangazi.

Lakinu sababu moja wapo ambayo inaashiria huenda dili hilo lisifanikiwe ni kutokuwepo kwa nahusiano mazuri baina ya Uturuki na Saud na Ozil ameonekana kuwa na mahusiano mazuri na Uturuki kuliko Saud.

Besiktas

Huku ndipo ana nafasi kubwa ya kuchezea na klabu nyingi zimeonsha nia ya kutamani saini yake.

Lakini tatizo ni aina ya mshahara ambao analipwa Arsenal, inakuwa ngumu kwao kuweza kumlipa.

Kwa wiki anapokea jumla ya Pauni 350,000, kiasi ambacho

Besiktas ni ngumu kuweza kukilipa ukilinganisha na klabu nyingine kutoka Marekani na Saud ambazo zinaweza kumlipa zaidi ya huo ili kumsainisha.

Lakini mbali ya mshahara sababu moja wapo ambayo itamfanya akubali kujiunga na klabu za Uturuki na mahusiano aliyokuwa nayo na nchini hiyo.

Fenerbahce SK

Timu nyingine kutoka Uturuki ambayo inatamani kuipata saini ya saini yake ni miamba hii ambayo anachezea Mtanzania Mbwana Samatta.

Fenerbahce ndio ilikuwa klabu ya kwanza kutoka nchini humo kuingia kwenye harakati za kuiwania saini ya Ozil.

Lakini bado shida inakuwa ni ilele ya mshahara ambao analipwa mchezajo huyu.

Kuna wakati alionekana kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu hii jambo lililozua ripoti nyingi kuwa huenda angetua hapo katika dirisha lililopita lakini ilishindikana.

Ingawa dili lilifeli wakati huo bado inabaki kuwa ni timu ambayo Ozil anaweza kutua na hapa kuna asilimua zaidi ya 50.

Inter Milan

Kocha wa timu hii Antonio Conte, amekuwa kwenye maboresho ya kikosi kwa muda mrefu ambapo amesajili wachezaji kadhaa wenye uwezo mkubwa.

Ripoti zinazodai kuondoka kwa Christian Eriksen kunatoa ishara ya miamba hiyo kuwa itaingia sokoni kutafuta kiungo mshambuliaji.

Ingawa chaguo la kwanza la Conte ni kiungo wa Chelesea NG’olo Kante, lakini uchezaji wa Kante unaokena kuwa tofauti na ule wa Ozil ambaye anauwezo mkubwa kuifanya timu ishambulie na kutengeneza nafasi nyingi tofauti na Kante ambaye ana akili ya kuzuia zaidi.

Pia bei ya Kante inaonekana kuwa kubwa tofauti na ile ya Ozil ambaye anaweza kupatikana bure katika dirisha lijalo la majira ya baridi.