Amunike: Tuna kila sababu ya kufuzu

Wednesday March 20 2019

 

By Thobias Sebastian

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike ameweka wazi kuwa timu yake ina kila sababu ya kufuzu.
Stars inawania nafasi ya kufuzu michuano ya Afcon ambayo imeshindwa kufanya hivyo zaidi ya miaka 30.
Amunike alisema wanacheza na timu nzuri Uganda ambayo imeshakata tiketi ya kucheza michuano hiyo lakini wamejipanga kwa hilo ili kupata ushindi na pointi dhidi yao.
Alisema tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki zetu ambao wanakila sababu ya wao kujitokeza kwa wingi na kushangilia ili kutupa nguvu ya kuwa na morali kwa wachezaji kushindana muda wote.
"Maandalizi ambayo tunaendelea kuyafanya ndio yananipa matumaini kuwa timu inaweza kufanya kile ambacho tunahitaji, lakini nimeongea na wachezaji wangu kusahau yale yaliyopita ila kurekebisha makosa ambayo tuliyafanya," alisema.
"Nawafahamu Uganda vya kutosha ni timu ngumu ambayo ina wachezaji wazuri kwa maana hiyo hautakuwa michezo rahisi ingawa kwetu tuna faida ya kucheza nyumbani na kama tuliweza kupata pointi kwao basi hapa kwetu linawezekana.
"Mechi iliyopita si kama tulikuwa tunacheza kwa kuzuia zaidi, lakini katika mechi hii ya nyumbani tutakuwa tunacheza kwa balansi kwa maana ya kuzuia na kushambulia sawa," alisema Amunike.

Advertisement