Ambokile wa Mbeya City aenda majaribio Misri

Muktasari:

  • Eliud Ambokile anashika nafasi ya pili katika ufungaji sawa na Said Dilunga (10), huku Herieter Makambo akiongoza akiwa na magoli 11.

Dar es Salaam. Mshambuliaji machachari wa Mbeya City, Eliud Ambokile yupo mbioni kutimkia nchini Misri kwenda kufanya majaribio.

Ambokile alionekana katika ofisi za TFF mchana wa leo akiwa na muwakilishi wake (Michael) ambaye anasimamia safari hiyo.

Hata hivyo Mwanaspoti lilipomfuata na kutaka kujua uwepo wake katika ofisi hizo licha ya jana kucheza mechi mkoani Mbeya, alisema yupo katika hatua za mwisho kwenda kufanya majaribio nchini Misri.

"Kaka ndio nimeingia na hapa na sikai kwa sababu natakiwa nikafuate viza ubalozi wa Misri na unakaribia kufungwa," alisema kwa kifupi.

Wakati huo huo alipoulizwa muwakilishi wake aliyejulikana kwa jina la Michael, alisema hawezi kutaja jina la timu kwa muda huu mpaka mambo yao yakamilike.

Eliud Ambokile anashika nafasi ya pili katika ufungaji sawa na Said Dilunga (10), huku Herieter Makambo akiongoza akiwa na magoli 11.