Ambokile aenda majaribio Misri

Muktasari:

Mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile mwenye mabao 10 kwenye ligi kuu Bara ana ofa nne za kufanya majaribio kutoka timu mbalimbali za Misri, Moroco, Tunisia na Afrika Kusini ambapo anapaswa kuchagua moja tu.

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Eliud Ambokile ameondoka nchini leo kuelekea nchini Misri tayari kwa ajili ya majaribio katika timu ya El Gouna FC inayoshiriki ligi Kuu nchini humo.
Eliud anatarajia kufanya majaribio ya siku tano na mara baada ya majibu kutoka kama yatakuwa mazuri anaweza kubaki katika timu hiyo lakini kama atashindwa ataondoka kuelekea Sauth Afrika kufanya majaribio katika timu nyingine ambayo bado haijajulikana.
Chanzo cha karibu kutoka kwa mchezaji huyo ambacho hakikutaka jina lake liwekwe wazi kilisema nyota huyo ambaye anamabao kumi katika klabu yake ya Mbeya City anatarajia kuanza majaribio yake kesho ambayo yatakuwa ni ya siku tano.
Kilisema kutokana na uwezo alionao mchezaji huyo wanaamini ataenda kufanya vizuri na atakuwa miongoni mwa nyota wa kitanzania watakaokuwa wanaiwakilisha nchi nje ya Tanzania.
"Kila kitu kitawekwa wazi maana timu nyingi zinamuhitaji kwa ajili ya majaribio, hatuwezi kumruhusu tu kuondoka wakati bado hatujapata barua rasmi ya mwaliko ingawa kuna maombi ambayo sio rasmi.