Alliance FC waibomoa tena Ndanda

Tuesday December 4 2018

 

By Masoud Masasi

KLABU ya Alliance imemchukua aliyekuwa kocha wa makipa kutoka Ndanda FC, Wilbert Mweta ikiwa ni moja ya mipango ya kuboresha benchi la ufundi kuwa na ufanisi mkubwa zaidi.

Hivi karibuni, Alliance ilimpa mkataba wa mwaka mmoja Kocha Mkuu, Malale Hamsini kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbwana Makatta aliyefunganishiwa virago baada ya kichapo dhidi ya Simba cha bao 5-1.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jackson Mwafulango alisema ujio wa kocha huyo utawasaidia wataalamu wa benchi hilo kuhakikisha wanafikia malengo kwa kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.

“Baada ya kumnasa Malale tuliona bado kuna haja ya kuwa na mtaalamu wa makipa, ndipo tulipomchukua, Mweta ujio wake ni sehemu ya kuimarisha benchi la ufundi la timu yetu,” alisema Mwafulango.

Kwa upande wa Mweta alifurahia kurudi nyumbani kwa kuwa yeye ni mwenyeji wa Mwanza na kuahidi kupambana kuona timu hiyo inafanya vizuri kwenye ligi.

“Nimefurahi kurudi nyumbani nitapambana kwa kushirikiana na wenzagu kwenye benchi la ufundi ili tufanye vyema zaidi.

Advertisement