Alliance FC, Prisons zachomoka mkiani

Muktasari:

Tangu ameanza kuinoa Prisons, Rishard ameiongoza timu hiyo katika michezo tisa, ikishinda sita, kutoka sare mara mbili huku ikipoteza miwili wakati Malale tangu aanze kuisimamia Alliance ameiongoza katika michezo 15 ikiibuka na ushindi mara sita, kutoka sare kwenye michezo mitano na kupoteza mechi nne.

ar es Salaam. Hakuna namna unayoweza kuwatenganisha kocha     na Mohammed ‘Adolf’ Rishard na ufufuko wa timu za Alliance FC na Prisons kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu.
Uamuzi wa timu hizo kuwapa majukumu ya kusimamia benchi la ufundi, umezaa matunda na kuzisaidia kutoka eneo la hatari kwenye msimamo wa ligi na kujiweka kando ya kundi la timu zinazokwepa kushuka daraja.
Ndani ya kipindi kifupi walichofanya kazi, makocha hao wamevuna idadi kubwa ya pointi ambazo zimefanya Prisons na Alliance kusogea kutoka chini ya msimamo wa ligi.
Alliance iliyopanda daraja mara ya kwanza msimu huu na inayonolewa na Malale, iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 36 wakati Prisons chini ya Rishard iko nafasi ya 12 ikiwa na pointi 32.
Malale alianza kuinoa Alliance Desemba, mwaka jana akijaza nafasi ya Mbwana Makata wakati Rishard alitua Prisons Januari akimpokea kocha Abdallah Mohammed.
Tangu ameanza kuinoa Prisons, Rishard ameiongoza timu hiyo katika michezo tisa, ikishinda sita, kutoka sare mara mbili huku ikipoteza miwili wakati Malale tangu aanze kuisimamia Alliance ameiongoza katika michezo 15 ikiibuka na ushindi mara sita, kutoka sare kwenye michezo mitano na kupoteza mechi nne. 
Alliance imeingiza mshambuliaji nyota Dickson Ambundo kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu. Ambundo ana mabao tisa.

Rekodi
Rishard aliitoka Prisons kutoka mkiani na kuiongoza kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0, ilitoka sare bao 1-1 na Alliance FC.
Prisons ilitoka suluhu na Ruvu Shooting, iliifunga Kagera Sugar mabao 2-0, iliichapa Mbao 2-1, iliifunga Stand United bao 1-0, iliilaza Azam 1-0 kabla ya kuichapa Mbeya City 1-0.
Alliance iliilaza Biashara United mabao 2-0 iliinyuka Ruvu Shooting 3-0, iliichapa African Lyon  2-0, iliifunga Mbeya City 2-1 kabla ya kuinyuka Lipuli 2-0.

Kauli za makocha
Rishard alisema mafanikio ya Prisons yametokana kwa kuwatengeneza wachezaji kisaikolojia.
“Wakati nafika timu  ilikuwa  haiko vibaya  sana niliona ina wachezaji wazuri hivyo nikaona inahitaji kubadilisha baadhi ya vitu ili iwe imara.
“Nilikaa na wachezaji wangu na kuwaambia neno moja tu kuwa wanaweza. Niliwambia jinsi walivyo na uwezo na yote yaliyotokea nyuma ni upepo mbaya ulipita.”alisema Rishard.
Hamsini alisema aliwajenga wachezaji wake ari ya kujiamini na kujua kuwa wanaweza kupata matokeo mazuri.
“Hii timu ni mpya kwenye ligi ina wachezaji wengi vijana nilichofanya ni kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutambua kuwa wanaweza kushinda mechi zilizopo mbele yao.
“Pia niliwambia kuwa ili timu isirudi katika ligi za madaraja ya chini lazima wajitahidi na kushinda mechi nyingi ili waendelee kucheza na wengine watasajiliwa na klabu kubwa,”alisema Malale.