Alex Ferguson, Ed Woodward wadaiwa kuzozana wakiwa jukwaani Bramall Lane

Muktasari:

Picha ziliwaonyesha wawili hao Ferguson na Woodward wakiwa kwenye mjadala mzito wakiwa jukwaani uwanjani hapo huku timu yao ikionyesha kiwango cha hovyo kabisa mchezoni. Picha hizo ziliwaonyesha wawili hao wakiwa kama wanakwaruzana kitu hivyo, Woodward akizungumza hadi kwa vitendo akionyesha mikono.

MANCHESTER, ENGLAND . GWIJI wa Manchester United, Sir Alex Ferguson na makamu mkurugenzi wa timu hiyo kwa sasa, Ed Woodward walionekana kuwa na mjadala mzito wakati timu yake ikicheza na Sheffield United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England juzi Jumapili.

Man United ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 huko Bramall Lane kabla ya kurudi kwa kasi wakafunga mara tatu na kuonekana kama wameshinda, lakini Oli McBurnie akaja kufunga bao kusawazisha na mechi kumalizika kwa sare ya 3-3.

Picha ziliwaonyesha wawili hao Ferguson na Woodward wakiwa kwenye mjadala mzito wakiwa jukwaani uwanjani hapo huku timu yao ikionyesha kiwango cha hovyo kabisa mchezoni. Picha hizo ziliwaonyesha wawili hao wakiwa kama wanakwaruzana kitu hivyo, Woodward akizungumza hadi kwa vitendo akionyesha mikono.

Baadaye picha zaidi za tukio hilo zilionekana wawili hao kama wamekubaliana kitu na kuwa na mazungumza ya kawaida na hata sura zao zilionekana kuwa na tabasamu.

Sheffield United iliiduwaza Man United kuwa kumiliki kipindi chote cha kwanza na kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha Man United alicharuka ikifunga mara tatu ndani ya dakika saba na kubadili mambo uwanjani kabla ya Oli McBurnie kufunga na kufanya timu hizo zigawane pointi. Kwa dakika 70, Man United ilicheza kwa kiwango cha hovyo sana kuliko hata kwenye mechi zile ilizochapwa dhidi ya Crystal Palace, West Ham na Bournemouth.

Mabao ya John Fleck na Lys Mousset yaliwafanya wenyeji kuongoza, lakini Man United ilifunga kupitia kwa Brandon Williams, Mason Greenwood na Marcus Rashford kabla ya Oli McBurnie, aliyetokea benchi kuja kusawazisha huku Woodward na Ferguson wakionekana kuchukizwa na timu hiyo kushindwa kupata ushindi muhimu wa ugenini kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Mashabiki wa Man United nao walichukia wakimtaka Kocha Ole Gunnar Solskjaer afukuzwe tu na timu akabidhiwe Mauricio Pochettino, ambaye kwa sasa hana timu baada ya kufutwa kazi na Tottenham Hotspur Jumanne iliyopita.