Aiyee, Dilunga wapewa dili

Muktasari:

  • Sababu ya pili aliyoitaja alisema ni kushindwa kujitambua na kuendana na kasi aliyoanza nayo huku akikosa mtu mzuri wa kumshauri.

HAKUNA utata straika wa Simba Meddie Kagere ndiye Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu huu, kwani mabao yake 23 ni vigumu kufikiwa kwa idadi ya mechi zilizosalia kabla msimu kufungwa, lakini mastraika wazawa wakapewa dili la akili kwa msimu ujao.

Salim Aiyee na Said Dilunga ambao wamekwama muda mrefu kufungwa kabla ya jana Aiyee kutupia moja, wamepewa mchongo wa kujipanga msimu ujao kwa kuhakikisha hawaridhiki mapema.

Aliyekuwa kocha wa zamani Yanga, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’ alisema kwa uzoefu wake wachezaji wengi hujisahau kwa wachezaji wenzake wanaocheza nao na mwishowe wanakuwa hawapewi ushirikiano.

Sababu ya pili aliyoitaja alisema ni kushindwa kujitambua na kuendana na kasi aliyoanza nayo huku akikosa mtu mzuri wa kumshauri.

Hata hivyo, Aiyee mwenye mabao 17 ambaye alikwama kufunga mabao kwa mufa mrefu, akiachwa na Kagere, alikiri kuchemsha kwa madai ya kukamiwa na mabeki wa timu pinzani lakini msimu ujao atajipanga vizuri zaidi.