Ahmed Jongo kuzikwa Tandika

Muktasari:

  • Aliyekuwa mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) Ahemed Jongo anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu majira ya saa saba maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam.

ALIYEWAHI kuwa Mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Ahmed Jongo amefariki dunia jana na anatarajiwa kuzikwa mchana wa leo Jumatatu kwenye makaburi ya Tandika, Dar es Salaam.

Mazishi ya Jongo anayekumbuka kwa umahiri wake wa kutangaza hasa mechi mbalimbali soka, atazikwa saa 7 mchana mara baada ya swala ya adhuhuri.

Kwa mujibu wa mtangazaji wenzake wa zamani na rafiki yake wa karibu, Charles Hillary marehemu Jongo kabla ya kukumbwa na mauti alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Hillary alisema Jongo alikuwa amelazwa hospitali ya Temeke na alikumbwa na mauti hayo jana na mazishi yake yafanyikia makaburi ya Tandika jirani na Bandari.

“Jongo alikuwa akiugua muda mrefu maradhi ya kisukari na alilazwa Temeke Hospitali kabla ya mauti kumkuta,” alisema Hillary, aliyetamba naye enzi hizo RTD sambamba na wakali wengine kama Mshindo Mkeyenge, Omary Jongo, Dominick Chilambo, Salim Mbonde, Abdallah Majura, Mikidadi Mahmoud, Ahmed Kipozi, Abdul Ngarawa na Barthlomew Komba.

Mtangazaji huyo alistaafu kufanya kazi RTD mwaka 2005.