Abraham anataka kuitema England, mzuka ni Nigeria

Muktasari:

Abraham, 21, ameichezea mara mbili timu ya Taifa ya England, lakini zilikuwa mechi za kirafiki, hivyo bado ana ruhusa ya kwenda kuitumikia timu nyingine ya taifa atakapohitaji. Tammy kwa sasa hataki kufikiria yaliyopita huko nyuma kilichopo kwenye akili yake ni kwenda kukipiga na Super Eagles.

LAGOS, NIGERIA. STRAIKA wa Chelsea, Tammy Abraham amesema hajafuta uwezekano wa kuichezea Nigeria katika soka la kimataifa licha ya kwamba, aligomea kufanya hivyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika Russia.

Fowadi huyo aliyekuwa kwa mkopo Aston Villa msimu uliopita, alisema bado anaweza kurudi kuichezea Nigeria kimataifa kwa kuwa ndiko asili yake.

Abraham, 21, ameichezea mara mbili timu ya Taifa ya England, lakini zilikuwa mechi za kirafiki, hivyo bado ana ruhusa ya kwenda kuitumikia timu nyingine ya taifa atakapohitaji. Tammy kwa sasa hataki kufikiria yaliyopita huko nyuma kilichopo kwenye akili yake ni kwenda kukipiga na Super Eagles.

Chanzo cha habari hiyo kimedai kwamba, Abraham mpango wake muhimu kwa sasa ni kuhamia moja kwa moja kwenye kikosi cha Nigeria katika soka la kimataifa.

Lakini, sasa kinachosubiriwa ni kuona kama ataweza kupenya na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza mbele ya washambuliaji Victor Osimhen, Paul Onuachu na Kelechi Iheanacho ambao wamewasha moto.