AS Vita wazuiwa Uwanja wa Taifa

Friday March 15 2019

 

By Charity James na Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Wakati joto la mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na AS Vita likizidi kupanda, wageni hao wamejikuta kwenye mzozo mkubwa wakati wakijiandaa kufanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Leo jioni msafara wa AS Vita ulizuiwa kwa muda kuingia Uwanja wa Taifa na kundi la watu wanaodaiwa ni makomandoo wa Simba kwa madai kuwa, kwenye basi walilokuwa wakilitumia alikuwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.
Hata hivyo, vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30
zilizimwa baada ya kutoonekana kwa Zahera kama ilivyokuwa
ikidaiwa na makomandoo hao.
As Vita waliingia uwanjani hapo wakiwa na magari mawili,
likiwemo basi la Simba ambalo limetolewa kwa wageni hao lakini,
katika kile kinachoelezwa kukwepa hujuma, basi hilo liliingia
likiwa na watu sita tu ambao, ni viongozi.
Kisha likawepo basi dogo ambalo ndilo lilitumika kuwabeba
wachezaji wa AS Vita.
Kwa habari zaidi kuhusu mzozo huo na kinachoendelea kwa sasa
uwanjani hapo, endelea kufuatia mitandao yetu ya kijamii.

Advertisement