AS Vita wajifua viwanja vya Gymkhana

Thursday March 14 2019

 

Kikosi cha As Vita ya Kongo kimeendelea kujifua katika Viwanja vya Gymkhana leo Alhamisi.

Kikosi hiko kilichokuwa chini ya kocha Florent Ibenge kilifanya mazoezi ya mbalimbali ikiwa ni mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba keshokutwa Jumamosi.

 Mazoezi ya kwanza yalikuwa ni kucheza mpira kwa haraka kila mchezaji anatakiwa kupasia pasi inayofika kwa mwenzake haraka.

Mazoezi ya pili yalikuwa ni kucheza ambapo aliwagawa katika maeneo matatu viungo sehemu yao, mabeki na mastraika.

Viungo ilikuwa kazi yao kupiga pasi kwa mastraika ambao kazi yao ilikuwa kuwazidi mabeki waliokuwa wanawakaba na kufunga.

Zoezi lingine ambalo walifanya ni mabeki kuanziwa mpira na kipa lakini hawakutakiwa kubutua bali walitakiwa kupasiana ili kuwatoka washambuliji ambao waliambiwa waanze kukaba kuanzia mbele.

Advertisement