AS Roma yampigia hesabu Batshuayi

Wednesday August 14 2019

 

Roma, Italia. Klabu AS Roma imeweka wazi kuhitaji kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi ili kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.

Sky Sport liliripoti kuwa, Roma tayari wameanza harakati za kuhakikisha wanamdaka mchezaji huyo wenye mkataba na Chelsea mpaka Juni 2021.

Roma wameripotiwa wanataka kufanya mazungumzo na Chelsea, licha ya mshambuliaji wao mwingine Edin Dzeko ataendelea kusalia katika kikosi hiko. 

Pia mshambuliaji huyu alikuwa akihusishwa kujiunga na Inter Milan lakini baada ya kusajiliwa kwa Romelu Lukaku ni kama dili hilo limepotea.

Batshuayi mwenye umri wa miaka 25, katika msimu uliopita alicheza kwa mkopo Valencia pamoja Crystal Palace.

Advertisement