AFCON 2021 majanga kwa Liverpool, Arsenal

Muktasari:

Uamuzi huo unaziacha klabu za Ligi Kuu England kuwa katika wakati mgumu kwa kuwakosa nyota wake katika mechi sita za mwanzo wa mwaka.

London, England. Liverpool uenda ikiwakosa Mohamed Salah na Sadio Mane msimu ujao kutokana na ratiba ya Kombe la Mataifa ya Afrika kurudishwa kuchezwa Januari-Februari badala ya Juni na Julai.

Kocha Jurgen Klopp atakuwa kwenye wakati mgumu Januari mwakani baada ya uamuzi wa CAF kurudisha mashindano Mataifa ya Afrika mwezi huo.

Mashindano hayo yapelekwa miezi ya katikati yam waka baada ya uamuzi wa Mkutano mkuu mwaka 2017 na mwaka 2019 nchini Misri yalifanyika Juni na Julai.

Hata hivyo, baada ya fainali moja mashindano hayo yamerudishwa Januari-Februari nchini Cameroon 2021.

Taarifa zilizotolewa jana Jumatano zinasema mkutano mkuu uliofanyika Yaounde, Cameroon, chini ya rais wa CAF, Ahmad Ahmad wamekubali kurudisha nyuma mashindano hayo.

Kwa mujibu wa Ahram Online, uamuzi huo umetokana kuangalia hali ya hewa kuwa nzuri zaidi mwanzoni mwa mwaka, pia wakiogopa kuingiliana na ratiba ya Kombe la Dunia la Klabu la Fifa litakalofanyika 2021.

Uamuzi huo unaziacha klabu za Ligi Kuu England kuwa katika wakati mgumu kwa kuwakosa nyota wake katika mechi sita za mwanzo wa mwaka.

Wachezaji watakaosekana mwakani.

Arsenal: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Nicolas Pepe (Ivory Coast)

Aston Villa: Ahmed Elmohamady (Egypt), Trezeguet (Egypt), Jonathan Kodjia (Ivory Coast)

Bournemouth: Hakuna

Brighton: Gaetan Bong (Cameroon), Leon Balogun (Nigeria), Yves Bissouma (Mali)

Burnley: Hakuna

Chelsea: Hakuna

Crystal Palace: Jeffrey Schlupp (Ghana), Cheikhou Kouyate (Senegal), Wilfried Zaha (Ivory Coast), Jordan Ayew (Ghana)

Everton: Jean-Philippe Gbamin (Ivory Coast), Beni Baningime (DR Congo), Oumar Niasse (Senegal), Alex Iwobi (Nigeria)

Leicester City: Daniel Amartey (Ghana), Wilfred Ndidi (Nigeria), Kelechi Iheanacho (Nigeria)

Liverpool: Naby Keita (Guinea), Sadio Mane (Senegal), Mohamed Salah (Egypt)