2018 New York Marathon yatimua vumbi

Muktasari:

Marekani inayowakilishwa na Bingwa mtetezi, Shalane Flanagan, inamtegemea mkimbiaji wao kutetea taji lake alilochukua mwaka jana, dhidi ya wakenya Vivian Cheruiyot na bingwa mara tatu, Mary Keitany, huku pia upinzani mkubwa ukitegemea kutoka kwa Mamitu Daska.

Nairobi, Kenya. Makala ya mwaka huu, ya  mbio za New York City Marathon, yameanza kutimua vumbi, muda huu katika jimbo la New York, nchini Marekani na kushirikisha wakimbiaji wapatao 21,000.
Majira ya Saa 11:20 jioni, kwa saa za Afrika mashariki, kipyenga kilipuzwa kuruhusu mbio za wanawake kuanza ambapo dakika ya kwanza tu, kumeonekana kuwa kwa upinzani mkubwa kati ya Kenya, Marekani na Ethiopia.
Marekani inayowakilishwa na Bingwa mtetezi, Shalane Flanagan, inamtegemea mkimbiaji wao kutetea taji lake alilochukua mwaka jana, dhidi ya wakenya Vivian Cheruiyot na bingwa mara tatu, Mary Keitany, huku pia upinzani mkubwa ukitegemea kutoka kwa Mamitu Daska.
Kwa upande wa mbio za wanaume, Bingwa mtetezi Geoffrey Kamworor atajitosa barabarani kupambana na Wakenya wenzake Wilson Kipasang na Daniel Wanjiru na Mtanzania Alphonse Simbu huku pia upinzani ukitarajiwa kutoka kwa Bernard Lagat wa Marekani.