20 kuiwakilisha Stars Chalenji

Muktasari:


Mashindano ya Chalenji yataanza kesho Disemba 7 na yatamalizika Disemba 9 yakichezwa katika viwanja viwili ambavyo ni Namboole na ule wa KCCA


Kampala. Wachezaji wawili watapunguzwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kitakachoshiriki Mashindano ya Chalenji yanayoshirikisha nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambayo yanaanza kesho nchini Uganda.

Kilimanjaro Stars ilikuja Uganda na kikosi cha wachezaji 22 lakini kanuni za mashindano hayo zinalazimisha kila timu kuwa na kikosi cha wachezaji 22.

Panga kama hilo halitowakuta wachezaji wa Kilimanjaro Stars tu bali hata ndugu zao wa Zanzibar 'Zanzibar Heroes' ambao nao wamekuja na kikosi chenye zaidi ya wachezaji 20.

Zanzibar Heroes ambayo ilitua hapa juzi Jumatano, ina kikosi cha wachezaji 25 na hivyo majina matano yatatakiwa kupunguzwa katika orodha yao ya jumla.

Nyota wanaocheza nafasi ya ushambuliaji na kiungo ndio wapo kwenye presha zaidi kutokana na idadi yao kuwa kubwa kuliko wa nafasi nyingine.

Katika kikosi hicho cha Kilimanjaro Stars kuna washambuliaji watano wakati wale wanaocheza nafasi ya kiungo wapo saba