20 Percent aja na nyimbo mpya Jieleze

Thursday August 30 2018

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongo fleva, Abbas Kinzasa '20 Percent' amekuja na ujio wa nyimbo mpya inayokwenda kwa jina la 'Jieleze' aliyosema ina ujumbe mzito kwa mashabiki wanaopenda kazi zake.

20 Percent aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Mali za urithi, Mbaya hana sababu, Money money na nyinginezo anasema bado anaamini nyimbo yake itafanya vizuri kutokana na ujumbe ambao ameuweka ndani yake.

"Gemu la muziki bado lipo wazi, sijaona wa kufanya niache kuimba, mimi naandika mashairi yanayoishi na ndio maana hata nyimbo zangu za zamani zikipigwa bado zinatikisa.

"Kikubwa nawaomba mashabiki wangu waendelee kuniunga mkono, huo wimbo wausikilize kwa umakini bila shaka vipo vitu watajifunza ndani yake ambavyo vina uhalisia wa maisha yetu ya kila siku,"anasema.

Mbali na ujio wa nyimbo hiyo anasema yupo kwenye harakati ya kuandaa filamu itakayoendana na kazi yake ya muziki na kwamba itakuwa ya kuigwa.

"Naanda filamu yangu ambayo itakuja kwa kishindo kikubwa na mashabiki watajua nilikuwa nafanya nini."

Advertisement