Yanga yabanwa mbavu

Muktasari:

Kipindi cha kwanza kimemalizika kwa suluhu kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Coastal Union katika pambano linalopigwa Uwanja wa Mkapa.

Kipindi cha kwanza kimemalizika kwa suluhu kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Coastal Union katika pambano linalopigwa Uwanja wa Mkapa.
Katika mechi hiyo wageni Coastal Union walionekana kuingia na plani nzuri ya kushambulia kwa kushtukiza na muda mwingi wakuwa vizuri kwenye kukaba.
Kocha wa Coastal Union, alikuwa akutumia zaidi upande wa kushoto alipokuwa anacheza Hance Masoud na Issa Abushe 'Messi' kuanzisha mashambulizi.
Wakati Masoud na Messi wakiwa wanafanya mashambulizi beki wa kulia, Hassan Kibailo na mabeki wengine watatu walikuwa awapandi mbele kushambulia.
Wachezaji hao walikuwa wakicheza hivyo ili kuwalinda washambuliaji wa Yanga, Tuisila Kisinda, Carmo Carlinhos na Yacouba Sogne ambao walionekana kuwa wasumbufu kutokana na uwezo wao wa kukimbia.
Wakati Coastal Union, wakionekana kufanikiwa upande wa Yanga kusuka mashambulizi walikuwa wanapitia wakati mgumu.
Yanga walionekana kuwa na nguzo imara ya ulinzi ambayo haikufanya makosa mengi hatarishi kama ambavyo viungo wao Feisal Salamu, Zawadi Mauya na Mukoko Tonombe walivyofajya vizuri.
Wakati viungo hao wa Yanga wakipeleka mashambulizi kwa mastraika wao ilionekana kuwa ngumu kupenya na zaidi walitumia mipira ya krosi ambazo zilipotea na nyingine kuokolewa.
Yanga wakijaribu kupitia pembeni walitengeza nafasi moja tu ambayo ilikuwa ya wazi iliyotokana na krosi ambayo Tonombe akiwa mwenyewe ndani ya boksi aliunganisha vibaya.
Wenyeji Yanga walipoharibu kupenya katikati ya Uwanja walikutana na ugumu wa viungo wa Coastal Union ambao muda mwingi walikuwa hawaoungui kwenye kufanya majukumu yao ya kukaba.
Mpaka kipindi cha kwanza wageni Coastal Union kutokana na plani zao walizoingia nazo walionekana kufaulu wakati Yanga walikuwa wakipata wakati mgumu kupenya.