Moto kuwaka EPL weekend hii, Lampard uso kwa uso na Klopp

Ligi kuu soka nchini England inarejea tena mwishoni mwa wiki hii baada ya wiki iliyopita kushuhudia mechi za ufunguzi wa msimu mpya wa ligi hiyo pendwa.

Jumapili hii kikosi cha Chelsea kitakuwa nyumbani (Darajani) kuwaalika mabingwa watetezi wa ligi hiyo Liverpool.

Timu hizi zinashuka dimbani zikiwa zimejikusanyia alama tatu kila moja baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya ufunguzi wa msimu.

Liverpool iliwachapa vijana wapya kwenye ligi hiyo Leeds United mabao 4-3 kwenye uwanja wa nyumbani na Chelsea waliivurumisha Brighton mabao 3-1 ugenini.

Je, Lampard na Chelsea yake wataweza kuizuia Liverpool ambayo imeanza ilipoishia msimu uliopita? Je, ni Werner au Mane atakayeibuka mbabe? vipi kuhusu Mo Salah ambaye alipiga hat-trick kwenye mchezo dhidi ya Leeds.

Tazama mechi hii kupitia SS Premier League namba 223 kwenye kifurushi cha Compact 49,000 tu. Piga *150*53 kulipia sasa kifurushi chako au piga 0659 070707 kujiunga na @dstvtanzania.