Schalke watavunja mwiko kwa Bayern Munich

Muktasari:

Bayern kupoteza katika mchezo wao wa ufunguzi kwenye Ligi Kuu ni ngumu, hivyo Schalke wana kazi ya ziada katika hilo.

LIGI Kuu ya Ujerumani 'Bundesliga' leo Ijumaa inaanza rasmi msimu mpya kwa kuzikutanisha mabingwa wa msimu uliopita, Bayern Munich dhidi ya Schalke 04 mchezo utakaopigwa Uwanja wa Allianz Arena.

Katika mchezo huu Bayern wanaingia wakiwa na imani kubwa kupitia rekodi yao kwamba hawajawahi kupoteza dhidi ya Schalke na katika mechi zao 21 za mashindano tofauti, Bayern alishinda mechi 18 na kutoka sare tatu.

Timu hizi kwa msimu huu ni mara ya kwanza kukutana katika ligi yao, msimu uliopita walikutana raundi za kawaida na Bayern Munich waliibuka na ushindi wa bao 3-0.

Pia Bayern haijawahi kupoteza mechi yao ya kwanza hivi karibuni, mara ya mwisho kupoteza ni msimu wa 2001/2002 dhidi ya Borussia Monchengladabach bao 0-1.

Schalke sio wababe mbele ya Bayern Munich kwani katika mechi zao 19 za mwisho kwenye Ligi Kuu, wametoka sare mitatu na kupoteza michezo 16 mbele ya mabingwa hao.