Bale anatua leo England

Muktasari:

WINGA wa Real Madrid, Gareth Bale anatarajia kutua nchini England leo ili kukamilisha usajili wake kwenda Tottenham Hotspurs katika dirisha hili baada ya miaka saba kupita tokea aondoke kwenda Madrid kwa dau la Pauni 86 milioni.

MADRID, HISPANIA

Bale mwenye umri wa miaka 31, atakuwa anajiunga Spurs kwa mkopo wa msimu mmoja ambapo itaigharimu timu hiyo Pauni 20 milioni kama ada ya usajili huo wa mkopo na mshahara wake kwa ambao ni Pauni 500,000 kwa wiki.

Madrid imekubali kumtoa kwa mkopo ili kuondoa gharama ya mshahara wake ambao inataka kuutumia kwa ajili ya kulipa wachezaji wengine na kufanya usajili wa wachezaji wapya.