Vyuma vitano hatari Manchester United

Muktasari:

Kocha Solskjaer baada ya kumsajili kiungo Donny van de Beek anataka timu ipiganie

MANCHESTER, ENGLAND

NI kweli Manchester United ilikuwa kwenye taratibu za mwisho za kukamalisha usajili wa winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ambapo ripoti zilieleza tayari ilishafanya makubaliano na wawakilishi wa Sancho na Dortmund.

Lakini kilichokuja kukwamisha dili hilo ni mkurungenzi wa ufundi wa miamba hiyo ya Ujerumani ambaye alisema kuwa wamefunga mjadala na winga huyo atachezea Dortmund kwa msimu huu.

Lakini kufeli kwenye dili hilo haikuifanyi United kuwa nje ya soko la usajili kwa kuwa kuna wachezaji watano ambao inaripotiwa kuwa wapo kwenye rada na huenda wakawasajili kabla ya dirisha hili kufugwa.

Mchezaji wa kwanza kwenye orodha hiyo ni Adama Traore kutoka pale Wolves na hiyo ni kwa sababu ya kauli ya kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye alisema kuwa baada ya dili la Sancho kukwama mpango mbadala ni kumsajili mchezaji mwingine kijana ambaye atakuwa na uwezo na kuifahamu vizuri EPL.

Na mchezaji huyo anatajwa kuwa ni Traore pekee ambaye anacheza katika eneo hilo la winga na anaifahamu vizuri EPL, ikiwa msimu uliopita alifunga mabao tisa na kutoa asisti 12.

Mwamba mwingine ni Alex Sandro, ambaye anacheza katika eneo la beki wa kushoto. Baada ya kumkosa Sergio Reguilon kutoka Real Madrid sasa nguvu imehamishia kwa mwamba kutoka Juventus ambaye anatazamiwa kuonyesha ushindani mkubwa dhidi ya mabeki waliopo ambao ni Luke Shaw na kinda Brandon Williams.

Sandro amecheza kwa miaka mitano pale Juventus na kufanikiwa kushinda mataji mara zote tano kwa sasa ana umri wa miaka 29.

Wakati Greenwood na Bruno Fernandes wanaonekana kuwa bora msimu uliopita, nyuma ya mafanikio hayo ilikuwa inatokana na ubora wa kiungo Nemanja Matic ambaye katika michezo 34 aliyocheza ni sita tu ndio United ilipoteza.

Dirisha United inataka kusajili Uros Racic kutoka Valencia ambaye inaamini kuwa inaweza akawa msaada mkubwa katika eneo hilo.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kuwa ni faida kubwa kwa United kwa mlinganisho wa umri wake na urefu wake wa futi sita na nchi nne sawa na Matic.

Kalidou Koulibaly ni jembe jingine lililo kwenye rada za United ambao wanataka aje kutengeneza ukuta wa chuma akishierikiana na nahodha Harry Maguire.

Mchezaji mwingine kwenye mipango ya kocha Solskjaer ni straika wa Inter Milan, Lautaro Martinez ambaye msimu uliopita ambapo amefanikiwa kufunga mabao 21 katika mechi 49.