Lamine, Carlinhos waongeza furaha Jangwani

Sunday September 13 2020

 

By Mwandishi Wetu

Mechi ya ushindani mkubwa kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City imemalizika kwa ushindi wa bao 1-0 lililowekwa wavuni kwa kichwa na beki Lamine Moro.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani, ujuzi na mashambulizi mengi imekuwa na mvuto baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare licha ya mashambulizi katika malango yote.

Yanga ilitumia silaha zake zote katika mechi hizo hadi pale Muangola Carlos Fernandez 'Carlinhos' alipoingia kipindi cha pili na kubadilisha mchezo iliyopelekea kupatikana kwa bao baada ya kupiga kona na Moro kuweka wavuni dakika ya 87 na kuwainua mashabiki waliolipuka kwa furaha na shangwe mithili ya nyuki.

Kwa ushindi huo wa leo, Yanga ambao walicheza na jezi zao mpya kwa mara ya kwanza wanafikisha alama 4 sawa na watani zao wa jadi Simba baada ya timu hizo kucheza michezo miwili kila mmoja.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa kwenye dimba hilo la mkapa

Mbeya City tofauti na mechi ya awali wakuokufa 4-0 dhidi ya KMC leo wameonyesha upinzani kwa kukaba na kushambulia.

Advertisement

Advertisement