Onyango atua na kusaini Simba

Muktasari:

BEKI mwenye mwili mkubwa vijana wa mjini hupenda kuita 'mwili jumba' anayetoka klabu ya Gor Mahia, Joshua Onyango (27) ametua nchini na kusaini mkataba wa miwili kuichezea Simba.

BEKI mwenye mwili mkubwa vijana wa mjini hupenda kuita 'mwili jumba' anayetoka klabu ya Gor Mahia, Joshua Onyango (27) ametua nchini na kusaini mkataba wa miwili kuichezea Simba.
Beki huyo ametua leo Ijumaa Agosti 14, 2020 saa 9:40 alasiri alitua nchini akitokea kwao Kenya ambapo amemalizana na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Beki huyo alitua nchini akiwa sambamba na Wakala wake, Agustino Ramadhan ambaye walikuwa wameongozana baada ya kushuka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na Shirika la Ndege la Precision Air wakitokea Arusha.
Onyango mwenye muonekanao wa mwili mkubwa baada ya kuwasili nchini walipokelewa na Mhasibu wa Simba, (Selemani)
Habari kutoka ndani ya Simba zilieleza kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba wa awali akiwa kwao Kenya ambapo sasa amemalizana ramsi na kutangazwa.
Onyango yupo kikosi cha kwanza timu ya Taifa ya Kenya (Harembee Stars), akicheza sambamba na Mussa Mohammed.
Kuwasili kwa Onyango nchini na kusaini mkataba kutaifanya Simba kuwa na mabeki wa kati sita ambao ni Pascal Wawa, Kennedy Juma, Tairone Santos, Yusuph Mlipili na Erasto Nyoni.
Ni wazi ujio wa Onyango utaongeza changamoto ya ushindani katika kikosi hicho cha mabingwa wa vikombe vitatu msimu huu hasa kwa Kennedy na Wawa ambao wamekuwa wakicheza mara kwa mara huku Nyoni akiwa kama mbadala wao.
Ujio wa Onyango pia utakuwa umewaweka pabaya mabeki  wawili wa kati Mlipili na Tairone ambao wanaweza kupewa taarifa za kuachwa kwenye kikosi hicho muda wowote.
Leo Ijumaa, Simba imetangaza nyota wapya wawili Onyango na Charles Ilanfya ambaye ni mshambuliaji akitokea KMC ambapo sasa wamefika nyota watatu wapya akiwemo Bernard Morrison kutoka Yanga.